Burudani

Mr T Touch: Ni vigumu kuwaepuka P Funk na Master Jay

Prodyuza Mr T Touch amedai ni vigumu kuyaepuka majina ya maprodyuza wakongwe, P Funk na Master Jay katika historia ya Bongo Flava hata akitokea prodyuza yeyote akafanya mambo makubwa zaidi.

Touch amesema si kwamba maprodyuza wa sasa hawafanyi kazi nzuri ya kuweza kupata heshima kama P Funk na Master Jay, bali wao wanapata heshima hiyo kubwa kwa sababu wao ni waanzilishi wa game.

“Master Jay na P Funk wanapewa hiyo sifa kwa kuwa wao wameanzisha game, kwa hiyo hata iweje hawezi akatokea mtu akaanzisha game leo hii, wapo ambao walishaanzisha game kwa hiyo wale heshima yao inabaiki kama ilivyo, hata mtu aje afanye nini ni lazima uwazungumzie P Funk na Master Jay, hata uje utengeneze hit songs zote za duniani,” ameiambia E News ya EATV na kuongeza.

“Hata watoto wetu tunaowazaa sasa hivi wakiwa maproduza watafuata historia, P Funk na Master Jay lazima watakuwepo tu, ipo hivyo miaka yote ni jambo ambalo haliwezi kufutika,” amesisitiza.

Mr T Touch ametengeza hits kama Bongo Bahati Mbaya ya Young Dee, Mazoea ya Bill Nass, Kibabe ya Professor Jay na nyinginezo kibao.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents