Habari

Mrembo aliyeruka kutoka ghorofa ya sita akimkimbia mbakaji atupwa jela

Mwanamke mmoja mjini Dubai amejikuta akiishia jela baada ya kuuguza majeraha aliyoyapata wakati akimkimbia mbakaji kwa kuruka nje ya chumba cha hoteli kilichokuwa ghorofa ya sita.

Ekaterina Stetsyuk

Mrembo huyo aitwaye Ekaterina Stetsyuk (22) ambaye kazi yake ni Mwanamitindo amesema alipatana na mwanaume mmoja mwenye uraia wa Pakistani ambaye ni mfanyabiashara wa vipodozi kuwa wakutane Dubai kwa ajili ya mazungumzo ya kumtangazia bidhaa zake.

Ekaterina kutoka Urusi amesema kuwa siku ya kwanza walipokutana katika Appartment hiyo ambayo mfanyabiashara huyo alikuwa amepangisha walizungumza kwa ufupi na baadaye kuanza kupata vinywaji.

Ekaterina Stetsyuk, 22, from the city of Irkutsk in eastern Siberia, has been left with serious injuries in hospital (pictured) after the fall

Mama mzazi wa Ekaterina ‘Inga’ amesema baada ya mfanyabiashara huyo kulewa alimpeleka hadi chumbani kwake ambapo alianza kumfosi kushiriki tendo la ndoa huku akimtishia kumuua.

Bi. Inga akizungumza na gazeti la Vatan wa Urusi amesema kuwa mwanaye aliamriwa avue nguo na mwanaume huyo ambaye alimwambia kuwa ana miaka 39 ,na alipokataa kufanya hivyo mwanaume huyo alimshikia kisu kutishia kumuua.

The model's mother has claimed Ekaterina had been held with a knife at her throat by an American man

Amesema baada ya purukushani Ekaterina alifanikiwa kumuangusha mwanaume huyo na ndipo alipopata mwanya wa kufungua dirisha na kuruka nje ambapo Polisi mjini Dubai wameeleza kuwa chumba hicho kilikuwa ghorofa ya sita.

Tulipigiwa simu na ubalozi wetu (Ubalozi wa Urusi) kuwa mtoto wetu amepata ajali ikabidi tuulize kilichomsibu lakini hatukupewa taarifa kamili hadi tuliposafiri kwenda Dubai,“ameendelea kusema Bi. Inda.

Kwa bahati nzuri tulimkuta anauwezo wa kuongea lakini alikuwa anashindwa kukaa, alitueleza kilichomsibu kuwa alikimbia mtu aliyekuwa anataka kumbaka, ambaye sisi alitutaarifu kuwa ni rafiki yake kibiashara,“amesema Inda.

Akitoa ushuhuda wa tukio hilo kwenye mahojiano na Polisi mjini Dubai Machi 21, 2018. Ekaterina amesema kuwa alishikiwa kisu na mwanaume huyo akimtaka avue nguo zote kitu ambacho alikataa katu.

Baada ya hapo ndipo alipoanza kuvutwa nywele kitu ambacho kilipelekea purukushani na akafanikiwa kumpokonya kisu mwanaume huyo.

Ekateria amesema alipofanikiwa kuchukua kisu mwanaume huyo alienda kufunga mlango huku akiambiwa kuwa ataletewa wanaume wambake endapo atajifanya jeuri, kauli ambayo ilimfanya akimbie kwa kutokea dirishani.

Polisi mjini Dubai wamesema siku ya tukio mwanaume huyo (Mfanyabiashara) alienda polisi kutoa taarifa kuwa amevamiwa na mwanamke akiwa kwenye chumba chake kwa kuchomwa kisu. Na kwenye taarifa yake alidai kuwa mwanamke huyo walikuwa wamepanga kufanya naye biashara na baada ya tukio hilo hakujua alipokimbilia.

Licha ya maelezo yote mawili, Eketarina ameshikiliwa na jeshi la polisi mjini Dubai kwa tuhuma za kujeruhi na kutaka kuuwa.

Eketerina amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye paja na mgongoni ambapo ndiyo maeneo yanayoripotiwa kuwa aliumia zaidi kwenye ajali hiyo.

Wazazi wa msichana huyo wamesema kuwa mtoto wao alikutana na mwanaume huyo kwa njia ya mtandao wa Instagram kabla ya kujenga mahusiano ya kibiashara.

Chanzo: Gazeti la Vatan

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents