Burudani

Mrembo Amber Rose avamiwa na kibaka

Video vixen anaelipwa mkwanja mrefu, Amber Rose amesema anahisi kuna mtu alimvamia nyumba kwake na kukaa takribani masaa manne huku yeye akiwa amelala.

Chanzo cha karibu na Amber kimeueleza mtandao kuwa, kibaka huyo alivamia nyumba ya Amber iliyopo maeneo ya San Fernando Valley, siku ya jumatano (jana),mapema asubuhi kwa kupitia dirishani, maeneo ya jikoni kisha kuingia kwenye baadhi ya vyumba.

Mmoja wa msaidizi wa Amber amesema kuwa wakati anaamka kuandaa chakula cha asubuhi, alikuta kioo cha dirisha la jikoni kimevunjwa na alama za miguu ambazo zilionyesha mtu huyo akijaribu kutaka kuingia chumbani kwa Amber.

Mapema leo Amber ambaye anaishi na mama yake, mtoto wake pamoja na walinzi wake mapema asubuhi waliwapigia simu polisi ambao walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa tukio hilo licha ya kubaini kutoibiwa kitu chochote.

Hii ni mara ya nne kwa Amber kuvamiwa na wezi akiwa amelala.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents