DStv Inogilee!

Mrembo Antu Mandoza kutoka Tanzania, asimulia jinsi alivyonusurika kwenye ajali ya ndege ya shirika la Ethiopian Airlines

Mtanzania Antu mandoza ambaye ni Muigizaji, Mtangazaji na Mjasiriamali pia, amefunguka namna alivyonusurika kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliyotokea leo asubuhi majira ya saa 2.

Antu Mandoza

Antu Mandoza kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa alitakiwa apande ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX ET302 lakini alibadilisha route na baadae akasikia taarifa za ajali ya ndege hiyo.

Antu anasema alipigiwa simu kibao kutoka kwa watu wake wa karibu wakimuulizia kama yupo hai, hii ni baada ya taarifa za ajli hiyo kusambaa mitandaoni.

Ajali hiyo ya ndege imeua watu wote (157) waliokuwemo kwenye ndege, hakuna Mtanzania hata mmoja, huku Kenya ikiwa na raia wengi 32 waliofariki kwenye ajali hiyo.

SOMA ZAIDI – http://bongo5.com/fahamu-mambo-8-kuhusu-ajali-ya-ndege-ya-ethiopian-airlines-ikiwemo-picha-za-eneo-ilipoanguka-na-mataifa-yaliyopoteza-watu-wengi-kwenye-ajali-hiyo-03-2019/

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW