Mrembo avunja mipango ya harusi yake na Jini kisa dawa za kulevya (+Video) 

Mwanadada Amethyst Realm kutoka Bristol nchini Uingereza amevunja mipango ya harusi na mpenzi wake ambaye ni pepo aliyemtaja kwa jina la Ray.

Amethyst Realm mwenye umri wa miaka 32 aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na pepo huyo wakati alipokuwa katika  ziara yake nchini Australia mwaka 2018, na wamekuwa pamoja tangu wakati huo kulingana na Daily Mail.

Wawili hao walikuwa wanapanga kufunga pingu za maisha lakini Amethyst aliamua kuvunja mipango hiyo baada ya pepo hilo kubadilika na kuanza kutumia dawa za kulevya.

Katika mahojiano kwenye shoo ya This Mornini UK akiwa ametokea Ureno, mrembo huyo alifichua kuwa mchumba wake alianza kujihusisha na kundi baya la watu na hata kuwaleta chumbani mwao.

“Kwa hivyo sasa, tumefuta harusi. Ilikuwa inaendelea vizuri hadi wakati tunaenda likizo na hiyo ilikuwa jana usiku na kisha akabadilika kabisa.

Kwa hivyo nafikiri alijihusisha na kundi baya. Alianza kutoweka kwa muda mrefu na wakati aliporejea alikuwa na roho nyingine,” alisimulia.

Amethyst alisema wakati mwingine walikuwa wanakaa pamoja bila kusemezana na kisha baadaye kumtupa nje na kusafisha nyumba yake.

Aliamini kuwa pepo hilo lilianza kutumia mihadarati na kuponda raha kupindukia licha ya kuliongelesha. Alisema kuwa familia ya Ray ilikerwa na habari hizo za kuvunja harusi yao lakini ilidai kuwa huenda hali ya jamaa yao ilitokana na janga la kimataifa kwani mazimiwi pia yanaogopa kuambukizwa virusi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW