Burudani

Mrembo na mtangazaji wa Uganda Flavia Tumusiime asimulia jinsi rapper J-Cole alivyotaka ‘kumla uroda’

Mtangazaji na mrembo wa Uganda, Flavia Tumusiime amesimulia kisa cha rapper wa Marekani, J-Cole aliyetaka kumla uroda.

uganda

Kupitia Facebook, hivi ndivyo alivyoandika:

Umeshawahi kujiuliza iwapo wakati mwingine tabia zetu hutoa dalili tofauti?

Mwaka 2012 niliposherehesha Big Brother Africa, niliweza pia kumhoji rapper wa Marekani, J-Cole. Nilikuwa nina hamu sana na mahojiano hayo kwasababu nilikuwa shabiki na nilijua nyimbo zake nyingi. Mahojiano yalienda vizuri sana, mimi na wenzangu tulienda kwenye show ya after party. J-Cole pia alikuja na timu yake na tuliombwa kupiga picha ya pamoja, tulifanya, lakini kama shabiki, niliomba tupige picha yangu na yeye na alikubali. Baada ya picha, aliniambia ‘shawty you look nice and I loved the interview’ lol, nadhani hivyo ndivyo rappers huongea.

10629848_1112299218787274_2196044684526822236_n

Tuliongea kwa muda, na kwa akili yangu nilidhani ilikuwa ni watu wawili wakifanya mazungumzo ya kikazi kuhusu muziki.

Kulikuwa na wasichana ambao walikuwa wamepangwa kukaa na kucheza naye, niliondoka na kuwaacha waendelee kufurahi, saa moja baadayE mmoja wa walinzi wake alikuja kwenye chumba chetu akiniomba nimfuate, kwamba alitaka kuongea na mimi kuhusu suala binafsi, wakati akinivuta, mwenzangu alikuja na kunishika mkono na kuniomba niongee naye. Alisema, “Ninahisi anataka muda wa faragha na wewe peke yake, usiwe mjinga, anadhani unapatikana.”

Flavia-and-J.Cole_

Nilishtushwa na hili na nilimwambia mlinzi aende na nilimuambiwa kuwa nilikuwa sawa hapa na kama kilikuwa ni kitu muhimu anaweza kuja kwetu. Niliendelea kushtushwa, ni kitu gani nilichomwonesha kilichomfanya aone kama nilitaka kwenda naye faragha?

Mwenzangu aliniambia, inabidi uwe makini sana jinsi unavyokuwa mbele ya watu, vicheko vya ziada, ishara ya mwili, maneno unayotumia yanaweza kutengeneza mtazamo usioutaka. Hadi leo natumia ushauri huu. Matendo yako yanaweza kuchochea jibu ambalo hujajiandaa nalo hivyo kuwa makini jinsi unavyojiweka kwa watu usiowajua, kuwa na uhakika na ishara unazozitoa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents