Burudani ya Michezo Live

Mrisho Mpoto aonya tukio la kigaidi Kenya ni changamoto ya kuboresha usalama wa Tanzania

Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto ameitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulichukulia tukio la kigaidi la Kenya kama changamoto ya kuboresha amani ya Taifa letu.

196771_10150159953216193_4779053_n
Mrisho Mpoto

Akizungumza na Bongo5 leo akiwa mkoani Mwanza, Mrisho alisema tukio hilo la kigaidi kwenye jengo la Westgate lililotokea Jumamosi nchini Kenya, linatakiwa lichukuliwe kama changamoto kwa Watanzania kujidhatiti kiusalama.

“Jukumu la usalama wa Tanzania nila kila Mtanzania, pia wakati umefika kwa serikali kuhakikisha inafuatilia watu ambao hawaishi kwa halali hapa nchini kwasababu makosa walioyafanya ndugu zetu wa Kenya hata sisi tunaweza kuyafanya kwahiyo tunatakiwa tuwe makini, alisema Mpoto.

“Bahati nzuri hili tukio halijatokea ndani kwetu ila ni bahati mbaya hili tukio limetokea kwa jirani zetu yaani barazani kwetu kwahiyo kama limeishia barazani tujitaidi tuliondani kutoka nje na kuangalia wenzetu walikosea wapi.”

Shambulio hilo lililofanywa na kundi la Al-Shabaab limesababisha vifo vya zaidi ya watu 70 na mamia wengine kujeruhiwa huku wengine hawajulikani walipo hadi sasa. Leo ni siku ya pili ya siku 3 za maombelezo yaliyotangazwa na Rais wa Uhuru Kenyatta kufuatia tukio hilo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW