Michezo

Mrisho Ngassa: Waleteni hao Yanga

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Azam Fc pamoja na Simba Sc, Kiungo wa Mbeya City, Mrisho Khalfani Ngassa, yupo tayari kuwavaa waajiri wake wa zamani, klabu ya Dar Young Afrika mchezo utakaokuwa muhimu kwa upande wa Yanga kwani inaitaji alama tatu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu.

Licha ya kutambua aliichezea kwa mafanikio makubwa waajiri wake hao wa zamani, klabu ya Yanga, ameweka wazi kuwa hatashangilia bao endapo atafunga katika mchezo wao utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi majira ya saa moja usiku.

Akizungumza, Ngassa alisema mafanikio makubwa ya soka aliyoyapata kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na klabu hiyo ya Jangwani, huku akisisitiza itakuwa ngumu kwake kushangilia bao endapo atafunga.

“Mpira ni kazi yangu na sasa nipo na Mbeya City ndio waajiri wangu naipenda timu yangu na nitahakikisha tunafanya kila liwezekanalo kuwafunga Yanga, lakini siwezi kushangilia nikifunga bao,” alisema.

Kiungo huyo alisisitiza kuwa ili kuweka heshima ni lazima awafunge Yanga, huku akiwataka Wanajangwani hao kutotegemea mteremko kutoka kwao Jumamosi.

“Mechi itakuwa ngumu kwa sababu Yanga watataka kushinda kutetea ubingwa, lakini pia na sisi tunataka kushinda ili kuweka heshima ndio maana tumejiandaa vya kutosha kuelekea katika mchezo huo,” alisema Ngassa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents