Burudani

Mrithi wa Adoph Mbinga apatikana

sELEMANI_sHAIBU2

African Stars Band “Twanga Pepeta” imefanikiwa kumpata mpiga Gitaa la Solo na Rhythm ili kuziba pengo la Adolph Mbinga aliyeondolewa ndani ya Bendi. Mpiga gitaa huyo ni  Selemani Shaibu Aliyetokea kwenye Bendi ya Akudo Impact Selemani ameshaanza kazi rasmi

ndani ya Bendi na anataraji kushirikiana vizuri na akina Miraji Shakashia, Godfrey Kanuti, Jojoo Jumanne na Hassan Kado. Twanga Pepeta kwa sasa ipo kwenye matayarisho ya kukamilisha kurekodi nyimbo 4 ili kukamilisha albamu ya nyimbo sita itakayozinduliwa hapo baadae mwaka huu na Selemani ameshiriki vilivyo kwa baadhi ya nyimbo zilizorekodiwa.

sELEMAN_sHAIBU

Nyimbo zinazotarajiwa kurekodiwa ni “Dunia Daraja” uliotungwa na Charlz Baba,” Penzi la shemeji” uliotungwa na Mwinjuma Muumini, “Mtoto wa Mwisho” uliotungwa na Ramadhani Athumani au Dogo Rama na “Umenivika Umasikini”  wa Luizer Mbutu.

Nyimbo hizi zitaunganishwa na nyingine mbili zilizorekodiwa hapo awali ambazo ni “Kiapo cha Mapenzi” uliotungwa na Saleh Kupaza na “Kauli” uliotungwa na Rogart Hegga wakati huo kabla ya kutimkia katika Bendi ya Extra Bongo.

n.b pix caption.

pix no 17 Selemani Shaibu akilicharaza gitaa la Rhythm katika onyesho la Twanga lililofanyika Bagamoyo tarehe 03-06-2011 katika ukumbi wa Palm Tree Beach Hotel. pix no 21 Selemani Sahibu kushoto na Miraji Shakashia wakicharaza magitaa katika onyesho la Twanga lililofanyika Bagamoyo tarehe 03-06-2011 katika ukumbi wa Palm Tree Beach Hotel.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents