Habari

Mrithi wa nafasi ya Dkt Elly Macha apatikana

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Mh. Catherine Nyakao Ruge kuwa mbunge viti maalumu kupitia tiketi ya Chadema.

Taarifa iliyotolewa ya NEC imesema kuwa imemteua Ruge baada ya kukamilisha kikao ilichokifanya leo.

Katika taarifa, imeelezwa kuwa kikao hicho kilifanywa kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Tanzania 1977 pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Soma Taarifa kamili:

Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikaochake cha tarehe 04 Mei, 2017imemteuaNduguCatherine NyakaoRuge kuwa Mbunge wa VitiMaalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujazanafasiiliyoachwawazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti MaalumMhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.

Imetolewaleo tarehe 04 Mei, 2017 na:-

Kailima, R.K

MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Uteuzi wa Ruge umefanyika baada aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Dk Elly Macha kufariki dunia Machi 31, mwaka huu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents