Habari

Msaada wa madawa na chakula wakwama katika nchi za Msumbiji,Malawi na Zimbabwe ikikadiriwa, zaidi ya watu mil 2.6 wameathirika (+ Video)

Maelfu ya watu hawana chakula wala sehemu ya kulala karibu wiki nzima baada ya kimbunga Idai kupiga pwani ya Msumbiji. Wakati jamii zilizoathiriwa zikiendelea kung’amua kiwango cha uharibifu uliofanywa na kimbunga hicho, nchi jirani zimeahidi kutoa msaada wa kibinadamu.

Kwa mujibu wa DW. Ingawa ukubwa wa hasara iliyotokea hautabainika hadi pale mafuriko yatakapokwisha, tayari Umoja wa Mataifa unaamini haya yatakuwa maafa makubwa zaidi kuwahi kusababishwa na kimbunga katika eneo la Kusini ya Ikweta. Watu wasiopungua milioni 2.6 katika mataifa ya Msumbiji, Malawi na Zimbabwe wameathirika.

Baada ya kimbunga hicho na mafuriko yaliyoharibu maelfu ya nyumba na hekari nyingi za mashamba ya kilimo. Kima cha maji ya mafuriko hayo kinazidi kupanda kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, na kukwamisha shughuli za uokozi. Idadi ya waliothibitishwa kuuawa na kimbunga Idai imefika watu 354 katika nchi hizo tatu, ikitarajiwa kuongezeka na kufika 1000.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents