Habari

Msaidizi wa Bernald Membe adaiwa kutekwa, Jeshi la polisi latoa tahadhari ‘Mtu anayeteka hakupi taarifa, Msitembee usiku kiholela’

Baada ya taarifa za kudaiwa kutekwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Allan Kiluvya ambaye pia anatajwa kuwa ni msaidizi wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Hatimaye jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni latoa kauli juu ya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu amesema, Amepata taarifa za tukio hilo kutoka kwa ndugu wa kijana huyo aliyetekwa. Na kuahidi kuwa jeshi la polisi linaendelea kufuatilia kujua kama kweli alitekwa au laahh.

Tumepata taarifa za tukio hilo kutoka kwa ndugu wa Allan, na sisi tunaendelea kulifuatilia kujua ni kwa namna gani alichukuliwa lakini siwezi kusema ametekwa kwa sababu bado hatujathibitisha“.amesema Kamanda Taibu kwenye mahojiano yake na EATV.

Kwa upande mwingine, Kamanda Taibu amewatahadharisha wananchi kuwa makini hasa nyakati za usiku, Ikiwemo kuacha safari zisizo na umuhimu ili kupunguza matukio ya namna hiyo.

Tukio la kutekwa kwa Allan limetokea usiku wa kuamkia jana Julai 6, 2019 alipokuwa na baadhi ya marafiki zake katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu aliyefahamika kwa jina moja tu la Magret, Ambaye pia ndiye aliyetoa taarifa polisi, amesema mara ya mwisho yeye na Allan walikuwa pamoja wakitokea eneo la starehe, kabla ya kutokea kwa watu wapatao 7, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo ndiyo ilimchukua na kuondoka naye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents