Msaidizi wa Waziri Mkuu wa Israel athibitika kuwa na virusi vya Corona

Msaidizi wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amethibitika kuwa na virusi vya Corona, maafisa wamesema leo, lakini haijafahamika mara moja iwapo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 70 ameambukizwa ama kazi yake itaathirika.

Israeli PM's aide tests positive for COVID-19

Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa maelekezo ya wizara ya afya, na kusema msaidizi huyo wa bunge ambaye vyombo vya habari nchini Israel vimemueleza kuwa yuko katika hali nzuri, atafanyiwa uchunguzi.

Kwa kawaida wizara ya afya inataka kutengwa kwa mtu anayeshukiwa kuwa na maambukizi kwa muda wa siku 14 na kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya corona mtu yeyote anayeonekana kuwa alikuwa karibu na mtu aliyeambukizwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW