Tupo Nawe

Msajili wa vyama vya siasa afunguka kukatwa jina la mgombea wa upinzani kwa kukosea kuandika ‘ACT Wazalendo’

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema malalamiko yanayotolewa na vyama vya siasa hususani upinzani, Kuhusu kuenguliwa kwa wagombea wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamesababishwa na wao wenyewe kushindwa kufuata sheria, kanuni na utaratibu.

Image result for Sisty Nyahoza"
Sisty Nyahoza

Akizungumzia fomu inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya mgombea mmoja ambaye amekatwa baada ya kuandika kwa kifupi Chama cha ‘ACT Wazalendo’, Nyahoza amesema kwamba chama hicho hakipo kwenye orodha ya msajili, Kwani kimesajiliwa kwa jina la ‘Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo)’ na sio ACT Wazalendo, kama mgombea huyo alivyojaza kwenye fomu hivyo hilo ni kosa.

Hiyo wanayosema ni kifupi ni kama ilivyo CCM kwa Chama Cha Mapinduzi, lakini huwezi kuandika CCM tu kwani inaweza ikawa inamaanisha kitu kingine. Sisi kama walezi siku zote tumekuwa tukiwasisitiza kuzisoma na kuzingatia sheria, lakini kama baba unasema na mtoto hafuati matokeo yake ndiyo hayo,” Amesema Nyahoza kwenye mahojiano yake na gazeti Mtanzania.

Kauli hiyo ya Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Imekuja ikiwa ni siku mbili sasa zimepita tangu vyama vya upinzani vikiwemo ACT Wazalendo na CHADEMA vitangaze kujitoa kwenye uchaguzi huo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW