Burudani

Msami adai kuwa na mashabiki wengi wa kike

By  | 

Mkali wa kudance na kuimba Bongo, Msami Baby anaye-hit na ngoma yake ya ‘Mdundo’ kwa  sasa ameeleza kuwa moja ya sababu za kucheza staili tofauti tofauti  katika nyimbo zake ni kwa sababu ya aina ya masabiki  aliona.

Akiongea katika DalaDala Beat ya Magic FM, msanii huyo ameeleza kuwa ana mashabiki wengi wa kike na watoto hivyo anajitahidi ku-balance aina ya uchezaji wake katika video.

” Katika video zangu na hakikisha na gusa kila mtu ndio maana nafanya hivyo, Mimi nina mashabiki wengi wa kike ambao ni watoto, wanafunzi wa chuo na wakina mama ambao wapo wengine wananifuata kuniambia niwa fundishe kudance,” amesema msanii huyo.

Pia akaongeza katika suala la kufundisha watu kucheza “Kwa sasa nina watu kama wanne kwa ajili ya training kuwafundisha kudance ili waweze kuwa fundishe kucheza.”

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments