Habari

Msando aomba kung’atuka ACT baada ya picha chafu na Gigy

Baada ya video chafu kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanasheria nguli, Albert Msando, ambaye pia alikuwa mshauri wa Chama cha ACT – Wazalendo, ameamua kujizulu wadhifa huo ili kulinda heshima ya chama hicho.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, kupitia facebook amedai amepokea taarifa ya mwanasheria huyo kuomba kujiuzulu.

Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, “kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka”.
Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
Act Wazalendo Msando Alberto Seif Abalhassan

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents