Burudani

Msanii aliyesainiwa na Hanscana, ‘MARIOO’ afunguka maisha yake yalivyokuwa ndani ya THT

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Marioo amesema licha ya kusainiwa na Hanscana lakini bado ana mahusiano mazuri na THT kwani hao ndio wamemuonesha njia hadi kufikia hapa alipo.

Akiongea na Bongo5, Marioo amesema kuwa THT ni kama nyumbani kwake kwani muda wowote akiamua kwenda anaenda na kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa awali.

Marioo jina lake limeanza kufahamika baada ya kuanza kufanya kazi na baadhi ya wasanii akiwemo Nandy, Christian Bella, Ditto, Mwasiti na wengineo.

_______________________________________________________________________________________________

Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App yetu ya Bongo5. Pakua sasa kupitia Play Store kwa kubonyeza link hii – https://bit.ly/2J2Argw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents