Burudani

Msanii huyu awa gumzo Kenya kwa kuachia wimbo unaowaponda mastaa wa muziki wanaoteswa na ufukara

Kwa wiki ya pili mfululizo msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kanda ya Pwani ya hapa Kenya, amezua gumzo kwenye vyombo vya habari mbalimbali na mitandao ya kijamii na kuleta hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wadau wamziki nchini.

https://www.youtube.com/watch?v=HFdd6zk_T4Y

Ni baada ya kutoa kibao kikali ambacho ujumbe wake unazungumzia maisha yake na ya wasanii wenzake wakiwemo legendary Nyota ndogo, Susumila, Sudi Boy, Chikuzee, Ali B na wengineo licha ya bidii wanayofanya kimUziki lakini mambo hayaja simama vyema kwa wengi wao.

Katika hit song hii ambayo inakwenda kwa jina ”Mziki Majanga, Dogo Richie aliamua kuusema ukweli mchungu uliopo kwenye game ya muziki sana sana inayohusu wasanii kutoka pwani ya Kenya.

Msanii Dogo Richy (Kushoto) akiwa na Mtangazaji wa kituo cha redio cha Citizen maarufu kama Mzazi Willy M Tuva. Photo Courtesy Richie Ree FB

Wakati idadi ya wasanii wa Afrila mashariki wanaofanikiwa kimaisha kutokana na pato la muziki ikizidi kuongezeka, Tanzania ikiwa inaongoza katika orodha hiyo, ni bayana pia kunao wengi wanaofanya vizuri kimuziki, nikimaanisha wanao toa hits baada ya hits na kutawala anga za muziki, lakini mwisho wa siku wanaishia kula makavu kama raia wengine.

Licha ya kuwa na majina makubwa kupitia muziki wengi mpaka sasa wanaishi nyumba za kupanga ilihali kunao wengine wanamiliki hadi mijengo na magari ya kifahari. Swala hili limeonekana kumkeketa nyongo msanii Dogo Richie aka Richy Ree, nakuona afadhali awasilishe malalamiko yake kupitia mziki ambao nimekusogezea hapa.

Sikiliza kibao hiki #MzikiMajanga.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Instagram: change_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents