Habari

Msanii kutoka Congo Aurlus Mabele afariki dunia kwa ugonjwa wa Kiharusi akiwa jijini Paris

Msanii kutoka Congo Aurlus Mabele afariki dunia kwa ugonjwa wa Kiharusi akiwa jijini Paris

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya Soukous Aurlus Mabele kutoka nchini Congo amefariki dunia jijini Paris nchini Ufaransa akiwa na miaka 67 huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kusababishwa na kiharusi licha ya kusemekana kusumbuliwa na Saratani ya Koo kwa miaka kadhaa sasa.

CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v62), quality = 85

Kwa mujibu wa NationBreaking Kifo cha Mabele kimetokana na kiharusi na Taarifa hiyo imetolewa na msanii mwenzake wa LOKETO Nyboma Mwandido.

Hata hivyo, Mwanamuziki mwenzake, Nyboma Mwandido amedai rafiki yake aliaga dunia usiku kuamkia Ijumaa baada ya kuugua kiharusi na maambukizi ya virusi vya corona.

Mwandido alisema kuwa, Mabele (67) alifariki wakati akitibiwa katika hospitali moja ya jijini Paris baada ya kulazwa usiku wa Alhamisi.
Aurlus Mabele alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi iliyovuma sana miaka ya 1990 ya Loketo, iliyoundwa katikati ya miaka ya 1980 pamoja na Mav Cacharel na Diblo Dibala.
Anajulikana zaidi kwa nyimbo zake zilizotamba zikiwemo Embargo, Liste Rouge na nyingine nyingi

https://www.youtube.com/watch?v=hfLVKv3bBec

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents