AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Msanii maarufu nchini Nigeria, Banky W afuata nyayo za Professor Jay na Sugu

Muigizaji, Muimbaji wa muziki na Mjasiriamali maarufu nchini Nigeria, Banky W ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Eti-Osa, Lagos nchini humo.

Related image
Banky W

Banky W ametangaza nia hiyo kupitia chama cha Modern Democratic Party (MDP) ambapo ameahidi kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu.

Akihojiwa na kituo cha runinga cha CNN, Banky W amesema kuwa “Kuna kundi kubwa la vijana nchini humo wanaongea na Ku-Tweet sana mitandaoni lakini hawachukui maamuzi. Kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya taifa la baadae. Nataka niwafundishe vitendo na kuwaelimisha namna Demokrasia ya kisasa inavyoweza kufanya kazi na kutengeneza Nigeria ya baadae,“.

Banky W anakuwa msanii mkubwa wa muziki nchini humo kujitosa kugombea Ubunge nchini humo.

Tayari wasanii wenzake, kama Davido amejitokeza hadharani kumpigia upatu kwenye uchaguzi Mkuu ujao Februari 16, 2019 .

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW