Habari

Mchekeshaji maarufu Somalia auawa Mogadishu

Msanii maarufu wa vichekesho nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Mogadishu na watu wawili wasiojulikana. Mpiango ya mazishi inaendelea.
Abdi Jeylani Marshale alikuwa maarufu kwenye vipindi vya televisheni na redio na ina arifiwa kuwa alikufa baada tu ya kutoka kwenye kituo cha redio ambako alikua anafanya shughuli zake za ucheshi.
Haijajulikana nani anahusika na mauaji hayo lakini mwaka jana marehemu aliwahi kutishiwa maisha na wapiganaji wa Al-Shabab.
Alikuwa maarufu kuchekesha watu huku akiigiza kama wapiganaji wa kiislam.
Walioshuhudia tukio hilo wameiambia team B5 Marshale alipigwa risasi mara kadhaa kichwani na kifuani na watu waliokuwa na bastola.
Baada ya tukio la kutishiwa na Al-Shabab, marehemu alikwenda eneo jirani la Somaliland siku kadhaa kujisalimisha kabla ya kurudi nyumbani.

Kwa kweli ni “siku ya huzuni leo kwenye tasnia ya sanaa na burudani Somalia na Africa, mchekeshaji Marshale alikuwa kiongozi wa sanaa ya uchekeshaji na kila mtu alikubali kazi zake. ” alisema Yusuf Keynan, mtangazaji wa Redio ya Kulmiye ambako Marshale alikuwa akifanya kazi.

Wakati huo huo inaripotiwa kuwa watu wawili wamejilipua nje ya lango la bunge mjini Mogadishu, na kumuua askari wa serikali na wao wenyewe.
Afisa wa polisi ameaambia waandishi wa habari kuwa watu hao walijilipua baada ya askari wa polisi kuwafyatulia risasi. Hakuna kundi lolote lilijitokeza kuhusika na shambulio hilo.

Tukio hilo limetokea wakati viongozi wa Somalia wakijadili juu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa vimelitimua kundi la al-Shabab nje ya Mogadishu lakini kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda mara nyingi limefanya mashambulizi katika mji huo.
Bado linadhibiti maeneo mengi kusini na katikati mwa Somalia.
Somalia haijawa na serikali thabiti tangu mwaka 1991.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents