Habari

Msanii mkongwe Cuba Gooding Sr afariki dunia

Mwanamuziki na muigizaji kutoka Marekani, Cuba Gooding Sr amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 72.

Mzee huyo ambaye ni baba wa muigizaji Cuba Gooding Jr amedaiwa kukutwa amefariki na kikosi cha moto akiwa katika gari lake lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara huko Woodland Hills, California.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, chanzo cha kifo hicho kimetokana na marehemu kuzidisha dawa ambapo kasha la dawa hizo lilikutwa kwenye gari lake likiwa tupu.


Picha ya gari la Cuba Gooding Sr ambalo amekutwa amefariki

Msanii huyo aliwahi kufanya vizuri na nyimbo zake zikiwemo ‘Everybody Plays The Fool’, ‘Just Don’t Want To Be lonely’ na nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents