Msanii mwenzetu kuzuiliwa Uwanja wa Ndege kisa kibali sio makubaliano yetu na Basata – Wakazi

Msanii mwenzetu kuzuiliwa Uwanja wa Ndege kisa kibali sio makubaliano yetu na Basata - Wakazi

Msanii wa mziki wa kizazi kipya Bongofleva Wakazi amefunguka juu ya kile kilichotokea juzi Uwanja wa Ndege baada ya Diamond Platnumz kuzuiliwa kwenda kufanya shoo nje ya nchi kisa hana kibali.

Wakazi amesema “Kanuni mpya ya Basata ya vibali tuliongelea kila kitu na ni haki kwa msanii kuwa na kibali lakini kuna maazimio tul;iwapa Basata wayapeleke kwenye Wizara husika,lakini pia kanuni hii ya kuwa unatakiwa uchukue kibali ukienda kufanya sho nje upitie kwao hicho ni kitu kigumu sana,cha msingi ni kwamba tukae chini na wasanii tunatakiwa kuhusishwa katika kila kitu maana kama kweli wanafanya kila kitu kwa ajili ya manufaa yetu basi iwe kweli mana sisi ndo wahusika wakuu”

lakini pia Wazi hakuishia hapo bali aliwausia wasanii kuwa na umoja na wawe na nia ya kushiriki kwa sababu “msanii anaweze akatokewa na tatizo wakati hakushiriki ila baada ya kupata tatizo asianze kupiga kelele na kuanza kuomba msaada”

Wakazi ameachia Ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la Kanda Maalumu aliyomshirikisha Nikki Mbishi.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW