Msanii Size 8 adai maombi ndio yamesimamisha ndoa yake

Msanii Size 8 ambae wiki mbili zilizopita amekua akiuguza vidonda vya maumivu ya mapenzi, baada ya kugundua kua mmewe Dj Mo ambae ni Dj maarufu wa muziki wa injili anatembea nje ya ndoa na muchepuko. Hali ambayo ilizua fujo na hoja kali kote mitandaoni na kufanya wanandoa hawa kutoelewana.

Lakini baada ya majuma mawili baadaye, Size 8 na Dj Mo wameonekana nikama wamerudiana na mambo yao yanaenda kama kawaida. Leo amejitoa kimasomaso nakufunguka kua siri kubwa ya kusimama tena kwa ndoa yao ni kufunga na kuomba kwake kwa siku tatu mfululizo na Mungu alisikia maombi yake hivyo hanabudi kumrudishia shukrani.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW