Burudani

Msanii wa Afrika apata dili la kushiriki wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 2018

Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imetangaza jina la mawili ya wasanii wakubwa wa muziki kutoka Marekani na Afrika kusini ambao wataimba wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 2018 uitwao ‘Colours’.

Jason Derulo na Cassper Nyovest

Taarifa kutoka mtandao wa Coca Cola Company umeeleza kuwa majina hayo ni Jason Derulo na Cassper Nyovest ambao wataimba wimbo huu wa ‘Colours’ ambao utakuwa sound track na ndio rekodi itakayotumika kuhamasisha FIFA World Cup 2018 itakayo chezwa sehemu zote dunani. Wimbo wa ‘Colours’ unatarajiwa kuachiwa rasmi mwezi Machi tarehe 16 mwaka huu amabo utakuwa na vionjo kutoka Afrika na Kilatini.

“I always get butterflies when I’m releasing a new song,”  ameelza Jason Derulo . “But this one feels different, It feels like such a perfect time for this record,” aeleza msanii huyo.

Kwa upande wa msimamizi wa project hiyo kutoka Coca Cola ndugu Brad Ross, amebainisha kuwa wamewaunganisha wasanii hao ili kuleta ubunifu na utogauti.

Kwa kushirikiana na Jason Derulo, Coca-Cola wamewatumia wasanii kutoka  Africa Kusini, Switzerland,  Saudi Arabia kutengeneza wimbo huo.

Kombe la dunia  2018 ilnatarajiwa kufanyika  ndani ya mwezi mmoja nchini Urusi  na zitaanza rasmi ifikapo mwezi Juni taraehe 14 na mechi za ufunguzi ni Saudia Arabia V/s Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents