DStv Inogilee!

Msanii wa Bongo Flava ampiga shabiki wake chupa!

Katika party iliyokua inafanyika Kigamboni wikiendi iliyopita, kituko cha aina yake kilitokea kwenye shughuli ambapo msanii Chibwa, aliyewahi kua kwenye kundi la Mexicana lacavera, alimpiga mmoja kati ya mashabiki zake na chupa baada ya ugomvi kuzuka ghafla.
Inasemekana shabiki huyo alikua anamtumia maneno machafu meneja wa Chibwa , na ndipo Chibwa kuingilia na kutaka kupooza mzuka wa huyo shabiki.

Shabiki alimgeuzia kibao Chibwa na kuanza kumshushia matusi na jamaa hasira zikampanda na kumpiga shabiki huyo na chupa.
Waliosadikika kuwepo kwenye tukio hilo ni pamoja Timbulo, na msanii Momba pamoja na Meneja.

Chibwa, baadaye alitafakari, na aliona kafanya makosa na baadaye kumfata tena Chibwa na kuomba msamaha pamoja na jeruhi lake na ndipo Chibwa kuamua kumsamehe na kugharamia matibabu ya shabiki wake.
Baada ya tukio hilo, Chibwa amewaomba mashabiki wake wote radhi pia.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW