Bongo Movie

Msanii wa Bongo movie nusura kufa kwenye ajali [Video]

Mwigizaji wa filamu ‘Bongo Movie’ Lawrence Anthony maarufu kwa jina la Makala, juzi amenusuruka kufa katika ajali ya basi la Champion ambayo ilitokea katikati ya Gairo na Morogoro. Makala amesema chanzo cha ajali hiyo, ni ukosefu wa umakini pindi dereva wa gari ku-over take lory na hatimaye kukutana na Lory lingine lenye trailer, hali iliyopelekea kurudi tena kwenye barabara yake na kumshinda na kuliingiza kwenye mtaro.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=cBUEXZX64Ac[/youtube]
Anasema gari lilianza kuserereka kwenye mitaro na baadaye kupondeka pondeka, lakini kwa bahati nzuri hakuna aliyefariki.
Kutokana na ajali hiyo hivi sasa msanii huyo amesema inamfanya aweweseke na kukosa usingizi kwa kuwa matukio kama hayo hayajawahi kumtokea, na hii imekuwa kama kumbukumbu kwa maisha yake hasa kwa mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents