Soka saa 24!

Msanii wa Hip Hop, Chance The Rapper auaga ukapera, afunga ndoa na mchumba wake wa utotoni

Msanii wa Hip Hop kutoka Marekani, Chance The Rapper wikiendi iliyopita amefunga ndoa mjini Newport, California na mchumba wake wa tangia utotoni, Kristen Corley .

Image result for chance the rapper wedding
Chance The Rapper na mkewe

Rapper Chance alimvisha pete ya uchumba, Corley mnamo July 4, 2018. Na harusi yake imehudhuriwa na Mastaa kibao wakiwemo Kanye West na Kim Kardashian.

Image result for chance the rapper wedding

Chance The Rapper alikutana na Corley kwa mara ya kwanza kwenye Party ya mama yake, muda huo Chance alikuwa na miaka 9 na urafiki wao ukaanzia hapo, na mpaka sasa ni miaka 16 imepita.

Siku hiyo, Corley alitumbuiza wimbo wa “Independent Women” wa kundi la Destiny’s Child.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW