Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Msanii wa Kenya ajitolea kumsaidia Wema Sepetu kupata ujauzito (+video)

Ni muda mrefu malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu amekuwa akitamani kupata mtoto – Hilo pia amewahi kuthibitisha wakati alipoongea na EATV.

Katika runinga hiyo Wema alisema, “Kiukweli napenda nimpate mtoto hata sasa hivi kwa sababu nimekuwa nikataka mtoto tokea na miaka 24 sasa hivi na miaka 29.”

Habari njema zinaweza zikawa zinamkaribia mrembo huyo kutokana na msanii kutoka nchini Kenya ambaye alikuwa anaishi Dubai, 2gb Diva amejitolea kumsaidia kupata mtoto ili kutimiza ndoto zake za muda mrefu.


                                                        2gb Diva

2gb Diva katika video ameonekana akimtaja Sepenga kwa kutaka kumsaidia kwa kusema, ” Wema Sepetu, sweetheart suluhisho tupo nalo. May be soon unaenda kuwa mama.”

Kwa sasa 2gb Diva anafanya vizuri na ngoma yake inayoitwa ‘Nikujue’ ambayo ameshirikiana na Zikki.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW