Burudani

Msanii wa Kenya Victoria Kimani kutumbuiza katika eviction show ya Big Brother wiki hii

Ikiwa imebaki siku moja kuifikia siku ya eviction katika shindano la Big Brother ‘The Chase’ huko Africa Kusini, tayari imefahamika kuwa dada wa rapper wa Kenya Bamboo aitwaye Victoria Kimani atatumbuiza katika show hiyo.

victoria-kimani2

Binti huyu mrembo ambaye pia amekua nominated katika tuzo za Nigeria Entertainment Awards 2013 katika kipengele cha the Most Promising Female Act zinazotarajiwa kufanyika New York, Marekani baadae mwaka huu, atasindikiza show hiyo Jumapili (June 9) ambayo itawapa jibu watanzania juu ya hatma ya mshiriki Feza Kessy ambaye yuko katika danger zone wiki hii.

Kimani ambaye muda wake mwingi amekuwa akifanya shughuli zake nchini Kenya, Nigeria na Marekani ameshafanya kazi na wanamuziki wakubwa duniani kama Busta Rhymes, Chris Brown na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents