Habari

Msanii aburuzwa mahakamani kwa kutoa wimbo unaokashfu kabila la Wakamba

Huwa inakuwa furaha pale msanii wa muziki yeyote duniani anapotoa wimbo mpya na kupokelewa vizuri na mashabiki wake lakini huwa mambo yanakuwa magumu zaidi pale wimbo huo unapokuwa na mistari yenye ukakasi au inayoleta taharuki kwenye jamii.

Hii imempata msanii wa muziki wa nyimbo za asili nchini Kenya,  John Gichiri Njau maarufu kama Isaiah kwa kuburuzwa mahakamani baada ya kuachia video ya wimbo wa Ikamba ambao maudhui yake yana lugha za kichochezi.

Msanii huyo ambaye kabila lake ni Mkikuyu, kwenye wimbo huo amesikika akisema kuwa mwaka huu kabila hilo litakula mbwa na ndege kwani maembe ambacho ni chakula chao kikubwa umeisha msimu wake.

Mwenyekiti wa Tume ya Ushirikiano wa Kitaifa nchini Kenya, Francis ole Kaparo amesema leo Machi 12, 2018 wamefanikiwa kumpeleka mahakamani msanii huyo.

Wimbo huo uliotoka wiki iliyopita, umetungwa kwa lengo la kuelimisha kabila la Wakikuyu kuacha tabia ya kukata miti hovyo kwa matumizi ya mkaa, umegeuka kuwa wimbo wa chuki kati ya makabila hayo mawili.

Maelfu ya Wakenya mitandaoni wameonekana kukerwa na wimbo huo huku wengi wakichukizwa na maamuzi ya kumburuza msanii huyo mahakamani.

https://youtu.be/b5Ny0QQ2Wkk

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents