DStv Inogilee!

Msanii wa Nigeria Kiss Daniel na producer wake wanusurika kifo kwenye ajali ya gari

Msanii wa Nigeria anayekuja juu kwa sasa Kiss Daniel amenusurika kifo kwenye ajali ya gari iliyotokea Jumatatu ya January 11 huko Lagos.

kiss daniel

Kiss Daniel alikuwa pamoja na producer wake DJ Coublon (aliyetengeneza Duro na Wash za Tekno) kwenye gari waliyopata nayo ajali, lakini wote wamenusurika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwimbaji huyo wa ‘Laye’, ambaye jina lake halisi ni Anidugbe Oluwatobiloba Daniel (21), ameelezea ajali ilivyotokea na kuwashukuru watu waliowaokoa, na kutoa ushauri kwa watu wasitumie simu wakiwa wanaendesha gari ili kisiwatokee kilichowatokea wao.

“Morning guys.. don’t press ur phone while driving fam, it’s never a good idea. Crashed into a canal last night @ lekki, all thanks to dese guys and some loyal fans that help get I and my producer out and the car… I wanna say a very big thank u to @djcoublon for screaming like a Yankee baby before the crash.. Bro u nailed it . We thank God, we still alive” aliandika Kiss Daniel.

DJ Coublon ndiye ametayarisha wimbo mpya wa Kiss Daniel uitwao ‘Good Time’.

Tazama moja ya nyimbo maarufu za Kiss Daniel – ‘Laye’

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW