Michezo

Ezequiel Lavezzi kulipwa mshahara mnono na klabu ya China

Mshambuliaji raia wa Argentina, Ezequiel Lavezzi mwenye umri wa miaka 31 ambaye ana kipiga katika klabu ya Paris St-Germain (PSG) chini ya kocha Laurent Blanc, anayehangaikia kupata namba katika kikosi hicho cha (PSG) amekubali dili kubwa la mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki kuichezea klabu ya Hebei China Fortune.

Ezequiel-Lavezzi-632522

Kwa mujibu wa gazeti la Times wawakilishi wa Lavezzi , walikuwa katika mazungumzo mara ya kwanza na Chelsea mwezi uliopita, lakini dili la kutua Stamford Bridge bado halijatoa muelekeo na badala yake amekubali kwenda China.

Mkataba wake na Paris St-Germain unamalizika mwisho wa msimu huu na Hebei China Fortune iliyopanda kucheza ligi kuu ya China msimu uliopita, imelipa pauni milioni 3.5.

Klabu hiyo ya China kupitia akaunti yake ya Weibo imetangaza kufanikisha dili hilo na kutamba kuwa kuwasili kwa Lavezzi kutaifanya kuwa na fowadi kiwembe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents