Michezo
Mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan akanusha kumtoa kafara rafiki yake
Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland, Asamoah Gyan amekanusha kumuua rapper ambaye ni rafiki yake kwaajili ya kafara.
Rapper Castro na mpenzi wake, Janet Bandu, walizama kufuatia ajali ya boti wakati wakiwa likizo na Gyan kwenye ufukwe wake huko Ada, kusini mwa Ghana.
Castro
Hata hivyo hadi leo polisi wameshindwa kuipata miili yao na hivyo kuwepo kwa tetesi kuwa maiti ya Castro ilitumika kishirikina kama njia ya Gyan kupata fedha zaidi. July 4 Gyan aliwaalika marafiki zake kwenye kiota cha Aqua Safari Resort, ambako walihudhuria watu zaidi ya 10.
Hata hivyo July 6, Castro na mpenzi wake Janet Bandu alichukua boti na kushindwa kurejea.