Habari

Mshauri wa Donald Trump atakiwa kujiuzulu

Serikali ya Donald Trump yaibua jipya. FT McFarland ambaye alikuwa naibu mshauri wa Rais wa Marekani, Trump ametakiwa kujiuzulu baada ya miezi mitatu tangu alipoteuliwa kukalia kiti hicho.

Mshauri huyo ambaye aliwahi kuwa mchanganuzi wa kituo cha habari cha Fox News ametakiwa kwenda kufanya kazi ya ubalozi wa Marekani nchini Singapore.

Imedaiwa kuwa hiyo inatokana na mshauri mkuu mpya wa usalama wa nchi hiyo Luteni Jenerali McMaster kuamua kulifanyia mabadiliko baraza lake la NSC ambalo liliteuliwa na mtangulizi wake Michael Flynn.

Flynn alijiuzulu mwezi Februari mwaka huu baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo kwa wiki pekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents