Habari

Mshauri wa Papa Francis ajiuzulu kwa kosa la kuwapa ndugu zake fedha ya Kanisa

Kadinali wa ngazi ya juu Vatican, Giovanni Angelo Becciu amejiuzulu ghafla bila kutarajiwa lakini imebainika kuwa aliambiwa na Papa Francis kufanya hivyo.

Cardinal Giovanni Angelo Becciu pictured with Pope Francis

Kadinali huyo alishukiwa kutoa fedha ya kanisa na kuwapa ndugu zake ingawa amekanusha kufanya kosa hilo.

Cardinal Becciu alikuwa mshauri wa karibu wa Papa Francis na awali katibu wa Vatican.

Alihusika na mkataba ambao una utata wa kuwekeza katika kujenga jengo la kifahari mjini London kwa kutumia fedha za kanisa.

Uwekezaji huo ulikuepo tangu waanze kumfanyia uchunguzi wa matumizi ya fedha.

Mtu kujiuzuru katika ngazi ya ukadinali ni jambo la nadra sana kutokea, taarifa kutoka ofisi ya baba mtakatifu zinasema.

“Baba mtakatifu amekubali maombi ya kujiuzulu yaliyowasilishwa na mwadhama kadinali Giovanni Angelo Becciu.”

Lakini kadinali huyo mwenye umri wa miaka 72, aliuambia mtandao wa Domani nchini Italia kuwa alilazimishwa kujiuzulu kwa sababu alishukiwa kutoa fedha za kanisa kwa kaka zake.

Giovanni Angelo Becciu from Italy, attends the courtesy visit of relatives following a consistory for the creation of new cardinals on June 28, 2018
Kadinali anasisitiza kuwa hakuiba hata euro moja

“Sijaiba hata euro moja. Sijafanyiwa uchunguzi lakini wakinipeleka mahakamani, nitajitetea mwenyewe kuwa sijaiba,” kadinali huyo alinukuliwa akisema hivyo.

Alizungumza baadae na vyombo vingine vya habari, kadinali alisema kuondolewa kwake kumekuja kwa kushtukiza. Alisema, Papa alikuwa na wakati mgumu sana kutoa taarifa hizo.

“Lilikuwa ni jambo la kushangaza. Mpaka jana… nilihisi kuwa rafiki wa papa, mtu wa karibu wa papa anayemwamini.

“Mara Papa akaniambia hana imani nami tena kwa sababu amepokea ripoti kutoka mahakamani kuwa nilifanya vitendo vya ubadhilifu wa fedha.”

Kadinali Becciu amesisitiza kuwa “hakueleweka”, akaongeza kuwa: “Niko tayari kueleza kila kitu kwa papa. Sijafanya jambo lolote baya. Nilimwambia papa kwanini anafanya hivi kwangu, mbele ya dunia nzima?”

Kadinali Becciu ni nani?

Giovanni Angelo Becciu, ni raia wa Italia ambaye amekuwa akitumikia ofisi ya huduma ya diplomasia ya Vatican.

Kuanzia mwaka 2011 mpaka 2018, kadinali Becciu alikuwa katibu mkuu wa Vatcan, wakati alipopewa jukumu la kumsaidia papa na shughuli zake za kila siku.

Cardinal Giovanni Angelo Becciu poses after a consistory ceremony lead by Pope Francis to create 14 new cardinals at St. Peters Basilica on June 28, 2018
Giovanni Angelo Becciu alipata ukadinali Juni, 2018

Ni papa Francis ndiye aliyempa ukadinali huo mwaka 2018, wakati alipochukua jukumu jipya la kusimamia idara inayoangazia maisha ya utakatifu.

“Ni mshtuko mkubwa kwangu na familia yangu na watu wa nchi yangu. Ninakubali kutii kutokana na upendo wangu wa kanisa na Papa,” vyombo vya habari vya Italia vimemnukuu Ijumaa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents