Michezo

Mshauri wa timu za vijana nchini, Kim Poulsen ang’atuka 

Aliyekuwa mshauri wa timu za vijana nchini, Kim Poulsen ameamua kuwachia ngazi kufuatia kukumbana na changamoto mbalimbali licha ya kufanya kazi hiyo kwa kipindi kirefu.

Kim ambaye amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu za taifa za vijana hapa nchini ameamua kujiuzuri nafasi hiyo ambayo ameitumikia tangu mwaka 2016.

Kim Poulsen ambaye ni raia wa Denmark ameanza kazi hapa nchini akiwa kocha Mkuu wa timu za Vijana mwaka 2011 na kupandishwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) mwezi Mei mwaka 2012 aliporithi mikoba ya Jan Poulsen.

Licha ya mkataba wa Kim kukatishwa mwaka 2014 ulipofika mwaka 2016 akawa mshauri wa ufundi kwa kushirikiana na aliyekuwa kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime na kuiwezesha Tanzania kucheza fainali za Afrika ikiwa ni kwa mara ya kwanza nchini Gabon mwaka 2017.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents