Michezo

Mshindi wa Bajaj zinazotolewa na SportPesa, Hatibu Mohamed aeleza ushindi ulivyobadilisha maisha yake

Ndugu Hatibu Mganga Mohamed (39) dereva kivuto Kigamboni alipokea habari za furaha alipopigiwa simu na timu ya SportPesa na kufahamishwa kuwa yeye ndiye mshindi wa 28 wa pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS KING DELUXE kutoka promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA.

Hatibu Mganga Mohamed akikabidhiwa Bajaj yake na SportPesa

Mshindi huyo alijawa na furaha kwani kipindi alichokuwa akipokea taarifa hizo alikuwa anapitia kipindi kigumu kidogo. Wakati akikabidhiwa zawadi yake, mshindi huyo aliipeleka timu ya SportPesa nyumbani kwake ambapo ni chumba kimoja kilichopigwa alama ya X nyekundu ikimaanisha inatakiwa kuvunjwa kwa madhumuni ya kupanua barabara.

Mshindi alisikika akisema, ameanza kuweka ubashiri na SportPesa ndani ya mwezi mmoja na alipopewa taarifa ya ushindi amepata matumaini kwani ingawa anatarajia kupoteza makazi yake, lakini kipato atakachopata kupitia biashara ya bajaji kitamsaidia kutunza familia yake na kulipia ada za shule za watoto wake wawili ambao wanasoma shule binafsi.

Mkazi huyo wa Ubungo Kibo alikuwa na ndugu, jamaa na marafiki ambao walifurahia ushindi wake na kuhamasika pia kuweka ubashiri na SportPesa kwani Promosheni hiyo ni ya kweli na Watanzania wote wana nafasi ya kujishindia TVS KING DELUXE kama yeye alivyoshinda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents