Habari

Mshindi wa Redd’s Miss Nyamagana 2013 (Mwanza) Diana Amimo avuliwa taji hilo baada ya kugundulika udanganyifu wa umri na uraia

Aliyekuwa mshindi katika shindano la kumtafuta mrembo wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Redd’s Miss Nyamagana 2013 Diana Amimo amevuliwa taji hilo baada ya kubainika kudanganya umri wake pamoja na urai, kasoro zilizompunguzia sifa za kuvaa taji hilo.

Diana Amimo
Diana Amimo (katikati)

Mratibu wa shindano hilo lililofanyika (May 11) jijini Mwanza, bwana Mukhsin Mambo wa Stoppers Entertainment, ameiambia Bongo5 kuwa baada ya kugundua mapungufu hayo kwa Diana, kamati ilikaa (June 6) na kuamua taji hilo kumvisha aliyekuwa mshindi wa pili Rosemary Peter ambaye sasa ndio Redd’s Miss Nyamagana 2013.

miss nyamagana
Rosemary Peter (Reds Miss Nyamagana 2013 wa sasa)

Mr. Mambo amesema udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza wiki moja baada ya shindano hilo, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo na kubaini kuwa Diana ni raia wa Kenya na ana umri wa miaka 17.

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents