Picha

Mshukiwa wa ulipuaji bomu mjini Boston, Marekani auawa, wa pili anasakwa

Mmoja wa washukiwa wawili wa tukio la ulipuaji bomu katika mbio za Marathon huko Boston, Marekani ameuawa kwa risasi huku polisi wakiendelea kumsaka mwingine.

http://www.youtube.com/watch?v=pX1593fM_y8

Polisi wa jimbo la Massachusetts wamewaonya wakazi wa Watertown, kujifungua ndani mwao na wasimfungulie milango mtu huyo anayeaminika kuwa ni gaidi. Wamesema mtu huyo ni hatari na ni tishio kwa kila mtu anayemsogelea.

Picha za washukiwa hao zimetolewa na FBI jana.

Tangazo hilo limekuja masaa kadhaa baada ya jana usIku kwenye mitaa ya Watertown kutokea tukio la kurushiana risasi ambaPo polisi mmoja aliuawa kwenye campus ya chuo cha teknolojia cha Massachusetts, MIT.

Kupitia akaunti yake ya Twitter (MASS STATE POLICE ‏@MassStatePolice) polisi wa jimbo hilo iliandika:

“If any concerns about someone at door, call 911 immediately. Repeat–Do not answer door, stay away from windows, keep doors locked.

Residents in and around Watertown should stay in their residences. Do NOT answer door unless it is an identified police officer.

Police will be going door by door, street by street, in and around Watertown. Police will be clearly identified. It is a fluid situation.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents