AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Msichana wa miaka 16 mwenye asili ya Nigeria/Canada apewa credit kwa kuproduce wimbo wa Jay Z katika album ya ‘Magna Carta Holy Grail’

Msichana wa miaka 16 mwenye asili ya Canada na Nigeria ni miongoni mwa ma producer walioweka mchango wa kuikamilisha most Anticipated album ‘Magna Carta Holy Grail’ ya Jay Z ambayo imetoka (July 4) kwa watumiaji wa simu za Samsung.

Wondagurl-1

Ebony Oshunrinde binti mwenye miaka 16 mwenye asili ya Canada na Nigeria amejikuta akiingia katika historia ya hip hop mogul Hov, baada ya beat aliyoitengeneza kutumika katika moja ya nyimbo zilizomo katika album hiyo kitu ambacho hata yeye hakukitegemea.

Oshunrinde ambaye amemaliza ‘grade 11’ katika shule moja huko Brampton, Canada amepewa credit kama producer aliyehusika kutengeneza beat ya wimbo unaoitwa “Crown” wa Jay Z.

Kwa mujibu wa Aceshowbiz Oshunrinde a.k.a WondaGurl aishiye Toronto alianza kujifunza u producer akiwa na miaka 9, na akiwa na miaka 15 alishinda shindano la ‘Battle of the Beatmakers’ huko Toronto lililompa exclusive management deal ya kusign na Black Box na baada ya hapo akaanza kufanya kazi na wasanii na maproducer mbalimbali wa Canada pamoja na Marekani akiwemo Travis Scott ambaye hufanya kazi na Jay Z na Kanye West.

Wondagurl-2

Mwanzo wa shavu la WondaGurl kuhusika katika album ya Hov, ilikuwa siku moja binti huyo alimtumia Scott beat aliyotengeneza na kama bahati wakati huo Jay Z alikuwepo studio na akaiskia beat hiyo.

Baada ya siku kadhaa Scott alimtumia Oshunrinde ujumbe kuwa kumwambia atayabadilisha maisha yake sababu beat yake itatumika katika album mpya ya ‘Magna Carta Holy Grail’, kitu ambacho hakuamini, “Usually that doesn’t really happen to 16-year-olds, I didn’t believe it at all, because it’s pretty crazy news.” Alisema binti huyo katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kama utani ndivyo ambavyo binti mwenye ndoto chanya amejikuta akipewa shavu kwenye album ‘kubwa’ ya hip hop mogul Jay Z, kitu ambacho naamini kitampeleka mbali, ukizingazia yuko nje ya Marekani na pia ni msichana na umri wake ni mdogo kupata mashavu ambayo huwa si rahisi sana kukutana nayo kwa watu maarufu kama Hov.

Oshunrinde hajapata nafasi ya kuonana na Jay Z lakini kwa mujibu wa binti huyo Jay Z anahamu ya kukutana naye hivi karibuni.

Album ya ‘Magna Carta Holy Grail’ inategemewa kutoka rasmi kesho (July 7) kwa soko la dunia baada ya kutoka (July 4) kwa watumiaji million 1 tu wa simu za Samsung.

Kazi kwenu maproducer wachanga wa kibongo au mtu yeyote mwenye kipaji chochote kutumia fursa za mtandao kujiunganisha na watu pamoja na kuonesha uwezo wa vipaji mlivyo navyo inaweza badilisha maisha bila kutarajia.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW