Burudani

Msimu wa 7 wa tuzo za ‘Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 wafunguliwa rasmi (+Video)

Jumatatu Disemba 02 , 2019. Baada ya kusibiri kwa muda mrefu hatimaye Africa Magic kwa kushirikiana na kampuni ya MultiChoice Africa, imetangaza rasmi kupokea maombi ya kushiriki kwenye msimu wa 7 wa tuzo za kimataifa za Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2019 maarufukama AMVCA Awards.

Akizungumza katika semina maalum kwaajili ya tuzo hizo za awamu ya saba na wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini, AfisaUhusiano wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Bi. Grace Mgaya amesemakuwa,“Baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu hatimaye tuzo hizi zimerejea tena kwa kishindo katika msimu huu ambao muda wa kukusanya kazi umeongezwa maradufu.

Tuzo hizi ni mahususi kwaajili ya filamu za Afrika na hufanyika kila mwaka ili kutambua jitihada kubwa za watengenezaji filamu, waigizaji pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika sekta hii ndani ya mwaka husika”.alisema Grace.

Naye AfisaMaendeleo ya filamu ,Bodi ya Filamu Tanzania ndugu Clarence Chelesi aliongeza kuwa, “Kampuni ya MultiChoice imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za wazalishaji wa filamu hapa nchini kwetu, hivyo nitoe rai yangu kwa magwiji wote wa filamu hapa Tanzania kuweza kutumia fursa hii adimu kwakushiriki katika mchakato huu ambao utawawezesha kujitangaza na kuzitangaza kazi zinazotengenezwa hapa nyumbani katika Nyanja za kimataifa kupitia tuzo hizi”,alielezaChelesi.

Maandalizikwaajili ya msimuhuu wa saba yanaendelea na tuzo hizi zitafanyika mnamo mwezi machi mwaka 2020 ili kuwapata vinara mbalimbali wa filamu kutoka barani Afrika.

Maombiyanayokaribishwakwaajili ya kushirikini ya kazi za filamu na televisheni ambazo zilitayarishwa na kuoneshwa kuanzia April 1, 2018 hadi Novemba 30, 2019.

Ufuataonimwongozo wa jinsi ya kutumakazikwaajili ya kushiriki:

Hatua ya 1: Andaa clip ya dakika 5 (reel) kwaajili ya online submission.

Hatuaya  2: Ingia kwenye tovuti ya Africa Magic kupitia www.africamagic.tv/AMVCA. na click kwenye banner ya AMVCA Seventh edition itakayo kupelekea kwenye ukurasa wa kutuma maombi

STEP 3: Jaza fomu za kuomba kushiriki halafu upload clip yako. Kila online submission iliyokamilika itapewa namba ya kumbukumbu kuthibitisha

STEP 4: Hakikisha video ya kazi yako inauzito usiozidi MB 300

STEP 5: Weka namba yako ya kumbukumbu ,kisha tuma hard drive ya kazi uliyoiwasilisha mtandaoni kwenda:

Margaret Mathore
2 nd floor, MNET offices
Local Production Studio
Jamhuri Grounds off Ngong road
Nairobi Kenya

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents