Burudani

Msimu wa pili wa tamthilia ya Empire kuanza kesho

Mifarakano ya kifamilia, mapenzi na harakati za kushika hatamu ziliifanya tamthilia ya hip hop ya Empire kuangaliwa zaidi kwenye kituo cha runinga cha Fox mwaka huu. Na sasa watazamaji wategemee uhondo zaidi kwenye msimu wa pili.

empire-season-2-guest-stars-kim-kardashian-justin-bieber-more-want-a-role

“Kama msimu wa kwanza ulijengwa kwenye mazingira ya nani atarithi kitu cha enzi, msimu wa pili ni falme zenye vita,” mtayarishaji mkuu na mwandishi wa tamthilia hiyo, Ilene Chaiken aliwaambia waandishi wa habari.

Empire inarejea tena hewani kesho Jumatano baada ya kuwa na wastani wa watazamaji milioni 17.3 kwa kila episode kwenye msimu uliopita.

Msimu wa pili unaanza miezi mitatu baada yaw a kwanza ulipoishia.

Lucios yupo jela kwa mauaji wakati mwanae Jamal (Jussie Smollett) anaongoza kampuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents