Habari

Msimu wa sikukuu; Jeshi la Polisi kuweka Askari nyumba za ibada

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litaimairisha ulinzi na usalama katika sikukuu Eid El Fitr inayotarajiwa kuwa mwishoni mwa wiki au mapema wiki ijayo na kuonya watakaofanya uhalifu kuchukuliwa hatua za kisheria huku jeshi hilo likijipanga kuweka nyumba zote za ibada ulinzi wa askari.

Akizungumza jijini Dar es saalam, Kaimu Kamanda wwa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lucas Mkondya amesema wamejipanga vizuri katika suala la ulinzi kwa wananchi.

“Tumejipanga vyema sana kwahiyo wananchi wajiandae vizuri na sherehe,jeshi liko vizuri tutakuwa na ulinzi wa kutosha askari watakuwepo wote hakuna askari atakae kuwa na sikukuu na tumepata askari wengine kutoka vikosi nje ya askari wa Kanda Maalum, ambao watakuja kushirikiana na nasi katika kuhakikisha kwamba kila sehemu ambapo kutakuwa na mkusanyiko wa watu askari watakuwepo wa kutosha,”alisema Kaimu Kamanda Mkondya.

“Lakini pia nyumba zote za ibada tutaweka askari tutakuwa na askari wa kawaida wenye uniform kutakuwa na askari kanzu kufuatilia nani anaetaka kufanya vurugu katika nyumba za ibada lakini pia katika sehemu ambazo wananchi wataenda kufanya sherehe tutahakikisha ulinzi unaimarishwa tutatumia vikosi vyetu vyote vya FFU, tutatumia hedkopta, mbwa na askari wetu wengi sana watakuwepo.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents