Msimu wa tuzo za Kili wazinduliwa

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro jana ilitangaza kudhamini tuzo za muziki za ‘Kill Music Awards’ kwa mwaka huu, huku kipengele cha fainali ya kusuniaka washindi wa kanda kikifutwa

na Dina Zubeiry




KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro jana ilitangaza kudhamini tuzo za muziki za ‘Kill Music Awards’ kwa mwaka huu, huku kipengele cha fainali ya kusaka washindi wa kanda kikifutwa.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza udhamini huo, jana kwenye Ukumbi wa DICC, jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo, alisema kwamba, wameondoa fainali za kanda ili kuharakisha kufanyika kwa mashindano ya mwaka huu, kama walivyoelekezwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Alisema, kazi ya upigaji kura kuwachagua wasanii watakaowania tuzo hizo, itaanza Mei 9 hadi Mei 28, kabla ya majaji kuangalia wasanii waliochaguliwa kama wako katika kundi stahili kwa ajili ya kupigiwa kura.

Aliongeza kuwa, uchaguaji huo utatumia njia ya barua pepe, ujumbe mfupi, ‘coupon’ zitakazokuwa kwenye magazeti.

Shelukindo alisema Juni 2, majaji watatangaza majina matano ya wasanii walioteuliwa kuwania tuzo hizo kwa kila kundi, ili wapigiwe kura, zoezi litakalofanyika hadi Juni 4.

Naye Mwakilishi wa BASATA, Angelo Luhala, aliwapongeza wadhamini wa tuzo hizo, kwani zimesaidia kukuza sanaa ya muziki nchini, kwa lengo la kutambua michango ya wanamuziki na washiriki wengine katika tasnia ya muziki.

Vipengele vitakavyowaniwa ni pamoja na mwimbaji bora wa kike, mwimbaji bora wa kiume, albamu bora ya taarabu, wimbo bora wa taarabu, wimbo bora wa Kiswahili (bendi), albamu bora ya Kiswahili (bendi), albamu bora ya R‘n’B, wimbo bora wa R‘n’B, wimbo bora wa asili ya Kitanzania, wimbo bora wa Hip Hop na albamu bora ya Hip Hop.

Nyingine ni wimbo bora wa Reggae/Ragga, albamu bora ya Afrika Mashariki, mtunzi bora wa muziki, mtayarishaji bora wa nyimbo, mtayarishaji bora wa video, mwanamuziki aliyechangia mafanikio makubwa na muda mrefu, wimbo bora wa Zouk na mwanamuziki/ kikundi bora kinachochipukia.


 


Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents