Habari

Msiogope baada ya giza nene asubuhi hutokea – Mh. Lema

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema ameeleza baada ya Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa kukamatwa akiwa katika mkutano wake katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa.

Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya mbunge huyo kukamatwa amesema kuwa wasiogpe baada ya giza nene asubuhi hutokea.

Msigwa amekamatwa na Polisi huko Iringa na kushushwa kwa nguvu jukwani ktk Mkutano halali. Msiogope baada ya giza nene asubuhi hutokea!

Mbunge Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano katika kata ya Mlandege huku akituhumiwa na kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents