Habari

Msomi aliyeteuliwa udiwani na Waziri Simbachawene aigaragaza Chadema

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Prof. Davis Mwamfupe
aliyeteuliwa kuwa Diwani wa Manispaa ya Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mhe George Simbachawene ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Dodoma kwa kumshinda Diwani wa Chadema.

Tokeo la picha la Davis Mwamfupe
Mhe George Simbachawene

Prof. Mwamfupe ambaye ni diwani wa CCM kwa kuteuliwa amemgaragaza Diwani wa kata ya Kikombo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndg Yona Kusaja kwa tofauti ya kura 50.

Uchaguzi huo umefanyika jana baada ya aliyekuwa Meya, Jaffar Mwanyemba kung’olewa madarakani baada ya kukutwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji wa Zuzu na matumizi mabaya ya Ofisi.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents