Michezo

Msosi wa sababisha kifo cha mtunisha misuli

Mtunisha mishuli maarufu Dallas McCarver ameripotiwa kufariki dunia nyumbani kwake Florida- Marekani baada ya kupaliwa na chakula usiku.

Dallas McCarver

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , ambao uliongea na mpenzi wa mtunisha misuli huyo Dana Brooke (26) anayecheza mieleka WWE, ameeleza kuwa aliongea na mpenzi wake huyo kabla ya umauti na alimwambia anampenda kabla ya kukata simu kwa ajili ya kujipikia chakula cha usiku.

Inasadikika kuwa kifo cha McCarver, kimesababishwa na kupaliwa na chakula hicho, hata hivyo mwili wake bado upo hospitalini kwa uchunguzi zaidi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents