Aisee DSTV!

Msuva ajifunga KMC FC kwa miaka miwili, kuitumikia miamba hiyo ya soka ya Kinondoni hadi 2021

Timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC imefanikiwa kumuongezea mkataba mshambuliaji wake, James Msuva ambapo sasa ataendelea kuwatumikia waajiri wake hao hadi mwaka 2021.

James Msuva ni mdogo wake na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva ambaye alijiunga na Waarabu hao Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga.

“Wakati tukiendelea na maandalizi ya KAGAME CUP leo James Msuva ameongeza mkataba wa miaka miwili na kuendelea kusalia KMC hadi mwaka 2021.“- KMC FC

James Msuva alijiunga na KMC akitokea katika klabu ya Mbao FC ya Mwanza kwa mkataba wa mwaka mmoja mwaka 2018

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW