Michezo

Msuva mchezaji bora Difaa Al Jadid

By  | 

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Difaa Al Jadid, Simon Happygod Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti ndani ya klabu ya Difaa Al Jadid ya nchini Morocco.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania,Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliyopita ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo inayojulikana kama Botola.

Msuva aliyejiunga na timu hiyo akitokea Dar es salaam Young Africans amekuwa akifanya vyema katika ligi hiyo huku akionekana tegemezi katika upachikaji mabao.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments